WANAWAKE WALIOZALIA NYUMBANI FAIDA ZAKE

FAIDA ZA KUOA BINTI ALIYEZALIA NYUMBANI.
1.Unamuoa wakati ameshapevuka kiakili tayari.( Hana utoto utoto)2. Atalea vizuri watoto mtakaoza kwa sababu ameshalea Mtoto wa kwanza kwa hiyo ana uzoefu.3. Anajua thamani thamani ya kupendwa kwa sababu alishawahi kutendwa.4. Hatatamani kukupoteza kwa sababu alishawahi kumpoteza ampendaye huko nyuma.5. Atajilinda Sana asikukosee kwa sababu ameshajifunza kupitia makosa aliyofanya huko nyuma.6. Akikukosea atakuwa mwepesi wa kuomba msamaha kwa sababu anajua hasara ya kutokuomba msamaha.7. Anajua thamani ya kuitwa Mrs fulani, kwa sababu aliwahi kuipata fursa hiyo akaipoteza, au huyo Mr fulani alimtumia vibaya.8. Anajua umuhimu wa kuwa mvumilivu, kwa sababu ameshajifunza na kujua kwamba kila mwanaume ana mapungufu yake hakuna mkamilifu.

Hawa watu wanafaa na wana haki ya kuolewa na kuwa na ndoa zao, kwa hata Mungu hutoa nafasi ya pili wakati mtu anamwendea na kumuomba msamaha.
Siyo kila mwanamke ALIYEZALIA nyumbani ni Malaya, Wengine walibakwa, Wengine kwa sababu ya ugumu wa maisha wakilazimika kuzaa wakiwa nyumbani.

NI MAONI YANGU TU SIKU NYINGINE NITATAJA HASARA AMBAZO NI CHACHE KULIKO FAIDA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *