UTI’s NI MOJA KATI YA MARADHI YANAYOWEZA KUHARIBU FIGO.

HIVO BASI NI VIZURI UFAHAMU JINSI UNAVOAMBUKIZWA NA JINSI GANI WAWEZA KUEPUKA–NI TATIZO LA MKOJO KUWA MCHAFU
Maambukizi katika njia ya mkojo au
katika kibovu cha mkojo, tatizo hili SI
miongoni mwa magonjwa ya zinaa
(STDs)
Mara nyingi tatizo hili husababishwa na
bacteria anajukanae kama E.coli ,
JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa watu hasa
wanawake hasa wenye uke kwa sababu
ya uwazi wa urethra kuwa karibu sana
uke na tundu la haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka tumboni na
kuingia katika njia ya mkojo urethra
kwa kuwafuta au kuwapangusa kutoka
kwenye huo uwazi wa uke na tundu la
haja kubwa.
Vile vile watu wenye uke (wanawake)
wana mrija mfupi sana wa urethra
(mrija wa mkojo) hivyo kwa sababu
hiyo ni rahisi kwa bacteria kusafiri na
kuingia kwenye kibovu cha mkojo na
kusababisha maambukizi.
Kibofu cha mkojo (bladder) ni kiungo
ambacho hutunza mkojo kabla ya mkojo
kuingizwa kwenye mrija urethra wake
ili utoke njekwa njia ya kukojoa.
NINI DALILI ZAKE
Dalili za maambukizi katika njia ya
mkojo (UTIs) kama yafuatayo;
 • –Kukojoa mara kwa mara kusiko kawaida;
 • —Maumivu kama ya kuwaka moto wakati
 • wa kukojoa (kama unaunguzwa na mkojo);
 • —Mkojo kutoa harufu isiyo ya kawaida;
 • –Mkojo kuwa na hali ya damu ndani yake;
 • —maumivu ya tumbo la chini mara nyingine;
 • Pia homa.
NINI MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi haya ya njia
ya mkojo hayatotibiwa mapema na
kimamilifu, maambukizi yanaweza
kusambaa mpaka kwenye mfumo wa
mkojo wa juu (kwenye kibofu na figo
kuathirika),
Na inapofikia hali hiyo ya maambukizi basi
inaweza kupelekea kulazwa hospitalini.
Pia, maumivu yanapokuwa ya hali ya
juu, hasa maumivu ya tumbo la chini,
mkojo kuwa na damu, haraka sana
mwone mhudumu wa afya
iwezekanavyo.
KUZUIA MAAMBUKIZI KWENYE NJIA
YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
 • —Kunywa mpaka glass sita za maji kwa siku;
 • —Kunywa kwa wingi juisi chachu ya Cranberry (jamii ya matunda Damu) 
 • Kojoa mara kwa mara kadiri iwezekavyo.
 • —Kojoa kabla na Baada ya tendo la ngono/ndoa
 • —Jipanguse/jisafishe kwa kutoka mbele kwenda nyuma mara baada ya kuoga au baada ya kujisaidia. (namaana wakati wa kuchamba basi ni vyema ukajisafisha kwa kupeleka nyuma na sio mbele upande wa uke ilipo urethra)
 • —Vaa chupi au nguo za ndani zisizo bana sana na hasa si vizuri kuvaa nguo za jamii ya nailoni, ni vizuri kuvaa nguzo za ndani jamii ya pamba ni nzuri zaidi.
 • —Oga Mara kwa Mara pia, kama unajua una Maambukizi katika njia ya mkojo basi fanya haya; Jizuie au acha kunywa chai, kahawa, mvinyo na vitu kama hivyo vyenye jamii ya alkali ndani yake.
 • –Jihadhari na juisi ya machungwa kwa sababu vyote hivyo hubadilika na kuwa alkali ndani ya mwili ambayo huchangia bacteria kukua ndani ya mwili asababishae UTIs
……
Imeandikwa na Dk.habelnoah

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *