Ubosi umenifanya nisiolewe, Umri Unazidi kusonga naombeni ushauri

#udakutz

Tangu nimalize harakati za masomo nimiaka 6 sasa. Wenzangu wote niliyokuwa nao amawameolewa na kupata watoto ama wamepata watotonje ya ndoa.Mimi tangu nikiwa mdogo na kwa maadiliniliyolelewa niliapa kutokuzaa nje ya ndoa. Lakinimpaka sasa nina miaka 33 sijapata mume wa kunioa.Mbaya zaidi kwa sasa nina cheo kazini kwangu, basikila mwanaume ananiogopa. Hapa nauona uzeeunasogea sina mume wala mtoto.Najiuliza, nivunje kiapo changu cha kutokuzaa nje yandoa ama niendelee kusubiria mume nisiyejuaatapatikana lini na huku umri unaenda?Niko njia panda jamani naombeni ushauri.#udakutz_

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *