TATIZO LA NGUVU ZA KIUME :

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu  havifanyi kazi vizuri, Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana. 
Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:
1. Kukosa hamu ya mapenzi; au 
2. Uume kusimama kwa uregevu; au 
3. Kuwahi kufika kileleni; au 
4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au 
5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; n.k
KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI
       Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona! 
        Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung’olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo. Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanawake wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana. 
.    
TUPO MOROCCO KINONDONI DAR ES SALAAM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *