NECESSARY LOSS

Kuna hatua fulani ikifika kwenye Maisha yako lazima ukubali Kitu kinaitwa “Necessary Loss” (Kupoteza kwa Lazima).Hii ni hatua ambayo unalazimika kupoteza KITU au WATU ili uvuke kwenda hatua nyingine.Mara nyingi ukifika hatua hii Ukiwa Mgumu kufanya hivyo utachelewa kwenda hatua inayofuata.
.
Kuna hatua ambazo utalazimika kuacha baadhi ya TABIA ili uvuke kwenda hatua inayofuata.Wakati huu ukifika wengi wanajua kabisa “Tabia fulani ndiyo inayonikwamisha” ila kwa sababu ameizoea anaendelea kuiishi.Matokeo yake kila siku anajikuta anabakia vilevile.
.
Kuna watu ambao wanatakiwa wapate “Necessary Loss” kwenye mahusiano yao.Kuna watu ni hatari kuendelea kuwa nao zaidi.Watu hawa unawajua kabisa,kinachofanya usiachane nao ni kukosa ujasiri na kuogopa maumivu ya kuachana nao.Wakati mwingine ni Hofu unajiuliza “Watanionaje?”.Ukiendelea kung’ang’ania kuwa karibu na watu ambao unajua unatakiwa UWE NAO MBALI-Lazima utakuja kujuta siku moja.Uwe jasiri kufanya unachopaswa.
.
Wakati mwingine unatakiwa upate “necessary loss” ya kuacha unachofanya ili uanze kufanya Kitu kingine.Umeshajua kabisa kuwa Njia uliyopo umepotea au Muda wa kuwa hapo umekwisha na unatakiwa kwenda mahali pengine au kuanza kitu kingine.Ila kwa sababu umezoea sana na imekuwa ni “comfort zone” yako hautaki kupoteza.Kumbuka kuna VITU VIPYA HAUWEZI KUPATA hadi utakapoamua KUACHANA NA ULIVYONAVYP SASA.
.
Sio kila UNAPOPOTEZA unapata HASARA kuna wakati unapoteza ili UPATE FAIDA KUBWA.Je,wewe kuna “necessary loss” yoyote unatakiwa kuifanya leo ili UPIGE HATUA?
.
See You At The Top
.
*Have a healthy and enjoyable Week….*

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *