MKE WANGU HAJUI KUWA NINAJUA

 Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nimeoa na nina watoto watatu na mke wangu , watoto ambao nimegundua sio wangu. Niliwahi kupata ajali mimi na rafiki zangu wawili, na mimi tu ndiye nilitoka hai, nilikaa kwa muda wa miezi 11 hospitali nikitibiwa, na daktari aliniambia kuwa sitaweza kupata watoto. Nikaamua kuokoka na kumkabidhi Mungu maisha yangu, baadaye nikaja kuwa mchungaji kwenye kanisa moja hapa Dar es salaam, ndipo nilipokutana na mke wangu, nikamuoa kwa taratibu zote. Sikuwahi kumwambia mke wangu tatizo langu kwa sababu niliamini kuwa Mungu atanifanyia muujiza wake na anataniponya. Baada ya mwaka mmoja wa ndoa yetu mke wangu akashika ujauzito akajifungua mtoto wa kiume. Maisha yakaendelea na mpaka watoto wakafika watatu. Nikawa siamini kama kweli Mungu amenitendea na kunipa watoto, nikaenda kupima DNA majibu yakatoka kuwa watoto wote sio wangu. Kinachonihuzunisha ni jinsi mke wangu anaenda kuhubiri kwa wanandoa wengine namna ya kuwa waaminifu kwenye ndoa zao, wakati anajua fika alichokifanya. Mke wangu mpaka sasa hajui kuwa ninajua watoto sio wangu. Naumia ndani ya nafsi yangu, najihisi mgeni ndani ya nyumba yangu. Nina uchungu mkubwa. Tafadhali nishaurini nifanye nini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *