MKE BORA NI YUPI?

Wakati Niko madrasa shekh alinikabidh niwafundishe watoto siku moja alikuja mtoto mmoja mdogo kujiandikisha ili ahifadhi Quran. Nikamuuliza je umehifadhi sura yeyote katika Quran tukufu?Yule mtoto akajibu ndio.Nikamwambia soma ulicho hifadhi katika Quran tukufu.Akasoma karibu juzuu amma yote.Nikashangazwa na kumuuliza je umehifadhi sura ya tabaarak?Akanijibu ndio.
Kisha nikamuuliza surati Anahl,akawa amesha hifadhi,alikuwa amehifadhi karibu sura zote katika Quran tukufu,nikashangazwa kwa mtoto wa umri wake kuhifadhi sura zote zile. Nikamuandikisha katika tahfeedh Quran kisha nikamwambia kesho njoo na baba  yako. Siku ya pili alipo kuja na baba yake nilishangazwa sana kumuona kwani mavazi yake alionyesha si mtu ambaye ameshikamana na dini kiasi cha kuwa na mtoto kama Yule. Yule baba wa mtoto akajuwa kuwa mimi nimeshangazwa akaniambia najuwa kama umeshangaa kwa kuwa mimi ni baba yake,lakini mimi nitakuelezea kwamba watoto wangu wote watatu wa kiume wamehifadhi Quran tukufu,na dada yao ana miaka minne amehifadhi juzuu amma. Lakini yote haya ni mke niliye kuwa naye ni bora kuliko wanaume alfu moja.Mke wangu, watoto wake wote wanapo anza kusema,huanza kuwahifadhisha Quran,na huwashindanisha kwa kuwaambia,Yule anaye hifadhi mwanzo sura anayo wapa basi yeye ndiye atachaguwa chakula gani kipikwe au kinunuliwe,na anaye maliza kuhifadhi juzuu moja mwanzo ndiyo atakaye chaguwa sehemu ya kwenda kutembea katika likizo ya wiki. Na wakati wa livu kubwa ya shule,mtoto aliye hifadhi sana kuliko wote ndiye atakaye chaguwa nchi gani twende tukatembea. Kwa kufanya hivyo watoto wakawa wanashindana na kuhifadhi Quran yote bila ya kuona tabu wala matatizo yeyote.Kwa hakika huyu ndio mke bora,ambaye ameiboresha nyumba yake. Na ndiye aliye tajwa na Mtume Swala lwahu alayhi wasalam katika hadithi yenye maana ya kwamba: Mwanamke huolewa kwa sababu nne, kwa mali yake,nasaba yake na uzuri wake na dini yake mchagueni aliyeshikamana na dini yake uwe salama (yaani usiharibikiwe katika maisha yako)Na akasema Mtume Swala Lwahu alayhi wasalam kwa maana ya kwamba:. Dunia ni starehe na starehe bora kuliko zote katika dunia hii ni mke bora. *NAWATAKIA SIKU NJEMA&MATAYARISHO MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI*

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *