MKE ALIMKASIRIKIA MAMA_MKWE_WAKE

*KISA KIZURI CHENYE MAFUNZO  Mke Alisimama Kwenye Meza Ya Chakula Na Kumuacha Mama Mkwe Wake Mzee Kwenye Meza Ya Kula. Mume Naye Alisimama Kwa Mshangao Ili Ajue Kwa Nini Mkewe Ameondoka Ghafla Kwenye Meza Ya Chakula…!!! 
*MUME*Kwa Nini Umeondoka Kwenye Meza Ya Chakula…? Mke Wangu Je Kuna Kitu Hakiku Kufurahisha…?
*MKE*Ndio Mimi Nahisi Mikono Ya Mamako Ni Michafu Jambo Hilo Limenitibua Nafsi Yangu Paka Nikapoteza Hamu Ya Kula.
*MUME*Je Hio Tuu Ndio Sababu Iliokuondosha Kwenye Meza Ya Chakula Au Kuna Mengine…? Haya Isiwe Tabu Niambie Tufanyeje Mke Wangu Kipenzi Changu Utakacho Sema Wewe Nitatekeleza. 
*MKE*Tumtengee Sehemu Yake Ale Peke Yake Kwani Kuanzia Leo Sipo Tayari Kula Na Mamako Meza Moja.
*MUME*Hapana Hapana Usiseme Hivyo Kipenzi Changu Haya Sawa Kuanzia Leo Tutamtengea Sehemu Yake Maalum Peke Yake Nakuahidi Mke Wangu. Lakini Inaonesha Hata Kuwepo Kwa Mamangu Pia Kunakudhoofisha Sio Mpenzi…? Au Tatizo Ni Hilo Moja Tu La Kunuka Kwa Mikono Ya Mamangu…?
*MKE*Haswaaa Mume Wangu Kiukweli Kuwepo Kwa Huyo Bikizee Ndani Ya Nyumba Yetu Kunaninyima Raha Kabisa.
*MUME*Lakini Mke Wangu Kama Unavyo Jua Mamangu Ni Mkubwa Kiumri Na Hana Mtu Wakumtegemea Zaidi Yangu Mimi Sasa Nini Rai Yaki…? 
*MKE*Ufumbuzi Upo Hapa Chakufanya Nikumpeleka Kwenye Nyumba Za Wazee Na Huko Ndiko Makao Yake Tena Atashughulikiwa Vizuri Sana Ila Kama Hutofanya Hivyo Basi Mimi Nitaondoka Na Sitorudi Tena Kwako…!!! 
*MUME*Wazo Zuri Sana Mke Wangu Muhimu Ni Furaha Yako Usijali Nitampeleka Mamangu Kwenye Nyumba Za Wazee 
Mke Alifurahishwa Na Maneno Ya Mumewe Na Mume Aliongea Huku Akimuonesha Tabasamu Mkewe. Mara Mume Akapigiwa Simu Na Baba Mkwe Wake Hapo Hapo Akamuuliza Mkewe Hivi Mke Wangu Unadhani Kwa Nini Babako Amenipigia Simu Na Amenitaka Kesho Wote Humu Ndani Twende Kwake…? 
*MKE*Ndio Najua Kwa Sababu Mimi Nilimwambia Baba Kila Kitu Na Akasema Atakupigia Simu 
*MUME*Kwa Sababu Gani Mke Wangu 
*MKE*Usijali Kesho Tukifika Kwa Baba Utajua Samahani Niko Hoi Taabani Naomba Uniache Nipumzike.
*MUME*Bila Samahani Mpenzi Lala Usingizi Wenye Afya. 
Mume Alitoka Kwenye Chumba Chao Na Akaelekea Chumbani Kwa Mamake 
*MAMA*Mwanangu Kwani Mkeo Ni Mgonjwa Maana Ameondoka Ghafla Kwenye Meza Ya Chakula Hadi Kashindwa Kumaliza Chakula Chake…? 
*MTOTO*Naaam Mama Mke Wangu Ni Mgonjwa Hali Yake Sio Nzuri Sana.
*MAMA*Aaah Mbona Umemuacha Peke Yake Umekuja Kwangu Hebu Harakisha Umpeleke Hospitali Au Ukamnunulie Dawa Mwanangu Tambua Kwamba Sio Vizuri Mkeo Alale Njaa Wakati Yuwaumwa. 
*MTOTO*Usijali Mamangu Mkweo Hayuko Taabani Sana Acha Ajipumzishe Kiasi Kisha Akiamka Nitamuandalia Chakula Ale. 
*MAMA*Alhamdulillah Kumbe Hali Yake Sio Mbaya Sana ALLAH Akuhifadhini Enyi Wanangu. 
*MTOTO*Allahummah Aamiin Mama Kesho Nitakupeleka Sehemu Na Kila Kitu Kitabadilika 
*MAMA*Wapi Tena Mwanangu 
*MTOTO*Usijali Mamangu Kesho Ikifika Utajua Tuu Ila Nakuomba Usibishe Wala Kunizui Kwa Kile Nitakacho Kifanya. 
*MAMA*Aaah Mwanangu Mbona Unanipa Wasi Wasi Hivyo Sawa Sitobishana Na Wewe Katika Maamuzi Yako Sababu Nafahamu Kwamba Wewe Ni Mtu Mwenye Hekima Na Busara.
Kesho Yake Saa Nne Asubuhi Mume Mke Na Mama Wa Mume Wanaenda Kwa Ukweni Kulipopigwa Simu Ili Kuitikia Wito. Mume Alimchukua Mamake Baada Ya Mkewe Kukataa Katakata Kuandamana Naye Kwao Ila Mume Alimjibu Mkewe 
*MUME*Usiwe Na Wasiwasi Mpenzi Wangu Acha Twende Naye Kwenu Baadae Tutampeleka Kule Tulipo Afikiana Jana           (Katika Nyumba Za Wazee)
*MKE*Alikubaliana Na Maamuzi Ya Mumewe Na Wakaenda Naye 
Walipofika Ukweni Walipokewa Vizuri Wakakaribishwa Na Wakaanza Kuongea Baina Yao. Iliadhiniwa Adhana Ya Sala Ya Adhuhuri Na Wakasali Kwa Pamoja. Na Kwenye Kusubiri Maandalizi Ya Chakula Cha Mchana Baba Mkwe Akaanza Kuongea Na Mkwe Wake Chemba. 
*BABA MKWE*Mkwe Wangu Kwa Hakika Nina Jambo La Muhimu Sana Lilo Nifanya Nikupigie Simu Uje Kwangu. Basi Acha Nikueleze Kama Unavyo Jua Mimi Nina Mtoto Mmoja Tuu Na Ni Huyu Mkeo Yeye Ndie Roho Yangu Na Kiukweli Siwezi Kumkatalia Kitu Chochote Kiudhati Mwanangu Alinipigia Simu Akiwa Katika Hali Ya Kutofurahishwa Na Uwepo Wa Mamako Hapo Nyumbani Na Jambo Hili Ni Haki Yake Kuchagua Nani Atakaye Ishi Naye Hapo Nyumbani. La Sivyo Binti Yangu Hatorudi Tena Kwako 
*MUME*Aaah Kumbe Simu Zote Wanamuongelea Mamangu Alijisemea Moyoni. Naaam Baba Mkwe Mbona Hili Swala Tushalitatua Tayari Mimi Na Mke Wangu Tumeamua Kumpeleka Mamangu Katika Nyumba Za Wazee Punde Tuu Tunapo Toka Hapa. 
*BABA MKWE*Ikiwa Mshakubaliana Natarajia Kwamba Tatizo Lishapata Ufumbuzi Alhamdulillah 
Chakula Kinaletwa Mezani Wakaja Wana Familia Wote Isipokuwa Mama Wa Mume Mke Akamnongonezea Mumewe Sikioni Mamako Atakula kule Store Usiwe Na Wasi Wasi Juu Yake Sawa Habibi
*MUME*Mke Wangu Wewe Ndie Uliye Sema Kwamba Mamangu Ale Kule Store…?
*MKE*Naaam Habibi Nimesema Ale Huko Kwani Kuna Tatizo…? 
Mume Aliiangalia Familia Ya Mkewe Walivyo Kaa Katika Meza Ya Chakula Kisha Akasema Mimi Siwezi Kula Pamoja Na Nyinyi Je Mwajua Sababu…? Kwa Sababu Mikono Yenu Ni Michafu Kama Zilivyo Nafsi Zenu. 
Wote Walishitushwa Na Maneno Yake Kisha Baba Mkwe Akasema Ndio Unaongea Nini Hivyo…? 
*MUME*Kwa Nini Moyo Wako Waugua Kama Vile Volcano Inataka Kulipuka Au Ni Kwa Sababu Ya Maneno Yangu…? 
Vile Vile Mimi Pia Jana Niliugua Sana Uliposema Kwamba Mikono Ya Mamangu Inanuka. Isitoshe Ukapiga Simu Kwenu Ili Iwe Mjadala Juu Ya Kumuondosha Mamangu Kwenye Nyumba Yangu 
Aliwaangalia Wakwe Zake Kisha Akasema Hivi Ni Sawa Kweli Nimpeleke Mamangu Kwenye Nyumba Za Wazee Kwa Sababu Binti Yenu Ameamua Hivyo…? Je Mutahisi Vipi Ima Nyinyi Pia Mkifikia Umri Mkubwa Kisha Mkataka Kufanyiwa Hivi…? Nasikitika Sana Juu Yenu Familia Mbaya Sana Msiokuwa Hata Na Chembe Cha Imani.
Mtoto Alimuita Mamake Mwenye Umri Mkubwa Alitoka Maskini Hata Hajui Chochote Kinacho Endealea Alimshika Mamake Huku Machozi Yanamtoka Akambusu Mikono Ma Kichwa Kisha Akainama Na Kubusu Miguu Ya Mamake Alafu Akamwambia Mamake…… Haya Twende Mamangu 
*MAMA*Twende Wapi Tena Wanangu…? 
*MTOTO*Twende Peponi Mtoto Akaanza Kulia Nakusema Ni Bebe Mamangu Unipeleke Peponi Kwa Radhi Zako Anamkumbatia Mamake Na Huku Wanatoka. 
Kabla Wafike Mlangoni Aliigeukia Familia Ya Mke Wake Na Akawambia…..Mimi Naipenda Pepo Yangu (Mamake) Na Nitakuwa Naye Popote Nilipo Ili Nifaulu Hapa Duniani Na Kesho Khera Nanyi Bakini Na Dunia Yenu (Binti Yao) Akatoka Na Mamake Wakarudi Nyumbani 
SHARE NA WENGINE WAONE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *