MAPISHI YA KUPIKA VILEJA VA MCHELE/RICE FLOUR COOKIES🍥

🍥VILEJA VA MCHELE/RICE FLOUR COOKIES🍥

MAHITAJI YA KUPIKA 🍥VILEJA VA MCHELE/RICE FLOUR COOKIES🍥

 • Samli ya kunukia Au upendavo 2 cups vijae  bila kuyayusha
 • Mayai 2 Makubwa
 • Unga wa Mchele ( Rice Flour) ule  mwepesi 6 cups  (nimetumia Measuring cup) vijae kidogo
 • Unga wa Mchele wa chenga (Ground Rice) 1- 1 1/2 cups inategemea  vipi unapenda kutafuna
 • Hiliki upendavo
 • Rose Essence /Arki ya mawardi Kiasi
 • Sukari 1 1/2 Cups 

JINSI YA KUPIKA VILEJA VA MCHELE/RICE FLOUR COOKIES🍥

 1. Sagaaaaaa Samli na Sukar mpaka iwe nyeupe kiasi 
 2. Alafu tia mayai  sagaaa alafu weka hiliki na Arki yako usage
 3. Anza kutia unga vikombe vitatu na wa chenga changanya kwa mkono
 4. Alafu malizia unga zote na ufinyinge uzuri uwe unashikana
 5. Fanya nakshi upendayo weka kidoto cha rangi panga kwenye tray and bake kwa dakika 20-25 havitakiwi vile brown iwe light kiasi
 6. Maliza vote panga sahanini mpaka wakati wa kula.

❗Note
Unga wa mchele ziko tofauti ya Brands
Ikiwa utaona haujakaza kufanyika shape basi nyunyizia kidogo dogo maji baridi mpaka uone umekaza na unaweza kufanya shape. 
Ukitaka kidogo gawa mara mbili ya kipimo na sukari utafanya moja kasorobo cup 3/4 kwa one cup Samli,,,,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *