MAPISHI YA KUPIKA TAMBI ZA KUKAANGA

MAHITAJI YA KUPIKA TAMBI ZA KUKAANGA

 • Tambi Nyembamba Pakti 1(150g)
 • Sukari Vijiko 4-5
 • Hiliki Kiasi
 • Arki Vanilla Tone
 • Zabibu Kavu Kiasi
 • Mafuta Ya Kukaangia vijiko 2 
 • Maji Glasi Kubwa 1 

MAANDALIZI YA TAMBI ZA KUKAANGA

Pasua tambi zako weka pembeni

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA KUKAANGA

 1. Weka mafuta kwenye sufuria anza kukaanga tambi zako mpaka ziwe na rangi ya brown
 2. Kisha weka maji,hiliki,sukari,zabibu na arki vanilla
 3. Koroga kidogo kuchanganya tambi zako
 4. Funika acha zichemke mpaka zikauke maji
 5. Changanya vizuri kisha pakua.


Angalizo


Ili tambi ziwe nzuri hakikisha maji hayawi mengi ili ziweze kuchambuka.


Unaweza kuongeza sukari kama mpenzi wa sukari

Enjoy:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *