MAPISHI YA KUPIKA NYAMA YA KUFUKIZA

Natumia nyama hii sana kama mishakaki nikipika urojo, ni very simple na super yummy , for me nachagua nyama hii kuliko mishakaki kwa urojo au mikate..

MAHITAJI YA KUPIKA NYAMA YA KUFUKIZA 

 • Nyama yoyote (nimetumia ya kondoo) nusu kg
 • Chumvi kiasi
 • Kitunguu saum 1 tbsp 
 • Tangawizi mbichi 1 tbsp
 • Pilipili manga ya unga 1 tsp
 • Uzile wa unga/bizari nyembamba 1 tbsp 
 • Garam masala 1 tsp 
 • Curry powder 1 tsp 
 • Maggi cube/kidonge cha supu 1

JINSI YA KUPIKA NYAMA YA KUFUKIZA 

 1. Ikate kate nyama kiasi kama za mishakaki, ikoshe itie kwenye sufuria  (nimetumia pressure cooker) , tia Kitunguu saum , tangawizi mbichi na chumvi kidogo, kumbuka unakuja kuweka maggi cube na ina chumvi so chumvi enyewe weka kidogo tu,  
 2. Iteleke nyama ichemke kidogo bila maji, mpaka ichanganyike, tia maji kiasi ya kuwivisha nyama pamoja na spices zote, funika wacha nyama iwive ikauke na ibaki na rojo kidogo na zito, wacha ipoe, 
 3. Chukua foel au kibakuli cha bati weka kaa la moto ndani na kitie ndani ya sufuria la nyama na kaa lake, tia drops kama 3 za mafuta ya kupikia , funika kwa dakika 2 au 3 , funua utoe mkaa ,na  ikoroge vizuri itie kwenye chombo na ENJOY 😋😋😋 very delicious na inasmell vizuri  i hope ukijaribu utapungua ile kuchoma nyama za mishakaki sometimes in shaa Allah.
 • unaweza kutia ukali  (ndimu)
 • unaweza kutia Pilipili boga/hoho inaongeza harufu nzuri, 
 • unaweza kutia pilipili ya kuwasha ukipenda 
 • zile drops za mafuta unazotia kwenye mkaa, ukipata mafuta ya ile nyama yenyewe inakua vizuri zaidi. SHARE NA WENGINE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *