MAPISHI YA KUPIKA MAANDAZI YA TUI LA NAZI

MAANDAZI YA TUI LA NAZIMAHITAJI YA KUPIKA MAANDAZI YA TUI LA NAZI

  • Unga 5 Vikombe
  • Tui la Nazi zito vugu vugu 1 ¼ kikombe
  • Sukari 3/4 kikombe cha chai
  • Samli iliyoyayushwa au mafuta 3 vijiko vya chakula
  • Hamira 2 Vijiko chai
  • Hiliki 1/2 Kijiko cha chai
  • Mafuta ya kukaangia

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI YA TUI LA NAZI1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
2. Pasha samli moto
3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto.
4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.
5. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke. *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15.
7. Sukuma madongo yakate. 
8. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.
9. Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *