MAPISHI YA KUPIKA KARA/ KAUKAU

KARA/ KAUKAU (design ya mzigo wa kuni ).

MAHITAJI YA KUPIKA KARA/ KAUKAU

  • Unga ngano ½
  • Chumvi kidogo na maji

JINSI YA KUPIKA  KARA/ KAUKAU

  1. kanda unga wako kidogo tu kwa maji na chumvi hauweki mafuta kisha kata vidonge vidogo vidogo  
  2. kisha sukuma kila kidonge kidogo tu kiweke pemben 
  3. vikifika 4_6 anza kuvipaka mafuta juu kisha vibebanishe ila cha juu usikipake mafuta visukume kwa pamoja iwe chapati moja kubwa sana kisha ibabue hio chapat kama unavyobabua manda za sambusa ikiondoa ubichi wote itoe 
  4. kisha zitenganishe zitoke idadi ya zile ulioziandaa kisha anza kuzikatakata kisha panga vile vifungu kama kimzigo cha kuni kisha chukua unga kidogo koroga na maji iwe rojo nzito chukua kipande kimoja kwenye vile vimizigo vyako anza kuzungushia ktkt kama unafunga kuni ila unapozungusha unakuwa unapaka ile rojo ya unga ili inate  vizuri isijiachie .
  5. kisha bandika mafuta jikon yakichemka dumbukiza mizigo yako ya kuni zikiwa blown toa weka katika chombo cha kuchuja mafuta hapo tayari pishi lako limekamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *