MAPISHI YA KUPIKA JEERA YOGHURT CHICKEN

JEERA YOGHURT CHICKEN :

MAHITAJI YA KUPIKA JEERA YOGHURT CHICKEN

 • Kuku 1 ( katakata vipande vya kawaida 8 mpaka 10)
 • Bizari Ya manjano nusu kijiko Cha chai 
 • Mafuta vijiko vya kulia 4
 • Mtindi kikombe 1
 • Uzile kijiko cha chai 1 Na nusu
 • Giligilani kijiko cha chai 1na nusu 
 • Vitunguu maji vi2
 • Kotmiri bunch 1 
 • Uzile mzima vijiko vya kulia 3
 • Mdalasini kijiti ki1
 • Pilipili manga vichembe 6
 • Karafuu 3
 • Pilipili mbichi za kijani 2
 • Vijiko vya chai vi2 vya tangawizi nA thom 
 • Spices mchanganyiko nusu kijiko.

JINSI YA KUPIKA JEERA YOGHURT CHICKEN

 1. Kataka vitunguu slices .
 2. Zikate pilipili mbichi mara 2.
 3. Weka mafuta katika sufuria halafu yakipata uvuguvugu weka pilipili mbichi ..
 4. Yakipata Moto kias weka Uzile mzima pilipilimanga nzima karafuu na mdalasini.
 5. Weka vitunguu Maji kaanga vitunguu mpaka viwe brown ..
 6. Weka Kuku uliemkata koroga koroga mpaka atakua amebadilika rangi..
 7. Weka tangawizi Na thom koroga koroga kidogo..
 8. Weka bizari Ya manjano uzile wa unga gilgilani ma chumvi..
 9. Koroga tena halafu weka mtindi funika iwive ikiwa tayari zima moto halafu weka kotmiri zikoroge vizuri ..weka katika sahani tayari kuliwa na wali mweupe 🍚👌😋

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *