MAPISHI YA KUPIKA FISH FINGER

*MAPISHI – FISH FINGER*Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.

MAHITAJI YA KUPIKA FISH FINGER

 • 500g Fileti ya samaki
 • 120g Chenga za mkate
 • 100g Unga wa ngano
 • Mayai 2
 • Ndimu 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Kotmiri
 • Mafuta ya kupikia

JINSI YA KUPIKA FISH FINGER

 1. Menya vitunguu saumu kisha visage
 2. Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu
 3. Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako
 4. Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.
 5. Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito
 6. Weka unga kwenye bakuli jingine.
 7. Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.
 8. Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).
 9. Epua na weka pembeni mafuta yote yakauke
 10. Weka kwenye sahani tayari kwa kula.

Enjoy! 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *