Mambo 5 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake

Kwenye suala la mahusiano ya kimapenzi kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuimarisha penzi na kulipa mizizi imara ili kuweza kudumu zaidi kama wapenzi watakuwa na nia moja. Leo tuangalie Mambo 5 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake.
❤💞❤1. Kukosolewa – “I think you are wrong”Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa. Wanachojali zaidi ni jinsi gani au njia gani imetumika kuwarekebisha. Mwanaume akikosea, anataka mpenzi wake amkosea lakini kwa mapenzi, sio kwa mikwaruzano au dharau au mbele ya kadamnasi. Mrekebishe au mkemee faragha, toa maoni yako na wala usimlazimishe, itamfanya aone unajali na unataka kumjenga.❤💞❤2. Kujali – “How was your day?”Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri💞❤💞3. Ucha Mungu – “Can we pray?”Mwanaume, anayesali au kutosali, lazima huwa ana imani kwamba Mungu yupo. Mwanamke mcha Mungu siku zote huwa ni wazo la kila mwanaume endapo ana mpango wa kuoa. Mwanaume huwa na amani kwa kiasi fulani akiongozwa na mwanamke wake kwa upande huo wa sala❤💞❤4. Msamaha – “I forgive you”Vikombe kwenye sahani havikosi kugongana, vivyo hivyo na kwa wapenzi, kuumizana hisia hakuepukiki, iwe kwa makusudi au bahati mbaya, mwenzio akikosea sasa isiwe ndo adhabu, akiomba msamaha ukamwambia nimekusamehe na kweli umemsamehe, funika kurasa endeleeni na maisha. Usililete tena mezani jambo ulilosema umesamehe💞❤💞5. Sifa – “That was great sex” Kama amefanya kazi nzuri, mwambie. Wote tunajua sio kila siku watu hufanya kiwango che Maradona au Pele, siku akiwa kwenye kiwango hicho hata yeye anajua, usisite kumpa sifa zake. Wazungu wanasema, ‘Yes, you can kiss and tell some of the times’. Na kama unaona kuna sehemu anahitaji kujisogeza, mwambie pia, tena kimahaba. Hii itawasaida nyote❤💞6. Upekee – “I admire you. No other man is like you” Ni kweli kwamba kuna wanaume ambao ni wazuri na wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo ulienaye, lakini kwake hujisikia vyema zaidi ukimwona yeye ni zaidi ya wote hao. Sio mbele ya macho yake tu, matendo yako na hata nyuma yake msifie kwamba yeye ndio mwanaume pekee duniani unayempenda na hakuna mwingine zaidi yake💞❤💞❤💞❤💞❤💞❤

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *