KWANINI MAPENZI YANAVUNJIKA PINDI MTU ANAPOGUNDUA AMESALITIWA..??

Na mwalimu Artist Jafa.
Mapenzi yanabebwa na MOYO na kwa vyovyote vile MAPENZI yanahitaji utulivu wa akili… Mtu yupo tayari kuvunja mahusiano aliyoyajenga kwa gharama ya MUDA NA MALI ili tu aitafute amani na furaha ya moyo wake, Mtu anaona ni bora kuanzisha mahusiano mapya ambayo hayajui ama anayajua na pengine anaingilia penzi la mtu mwingine ikiwa tu anaongozwa na moyo kufanya hivyo, UNADHANI NI KWANINI?
Usalama wa PENZI upo kwenye maneno yenye kuujenga moyo, Ni kweli kabisa NI BORA KUUPA UTULIVU MOYO WAKO kuliko kuyaishi mateso ambayo hujui yatakwisha lini, Kinachoumiza MOYO ni kuona kila unaloweza kumfanyia mpenzi wako ili ajione ana thamani duniani lakini kwake ni kama kumletea kitumbua tu wakati anawazia SAMBUSA! Mapenzi ni yale yale ambayo waliyaishi wazazi wetu ila tofauti iko kwenye NAMNA GANI MWENZA WAKO ANAKUCHUKULIA.
Jifunze kuenenda na MOYO wako unavyotaka lakini ukiona AKILI yako inakataa jambo usiwe mjinga kudhani akili itakupotosha, MOYO ukihangaika kumbuka AKILI nayo inachoka na mwisho wa siku utakuja kumchukia kila mmoja na utabaki kuwa wakuokota okota tu.
BE CAREFULLY ABOUT LOVE.
UMRI HAURUDI NYUMA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *