JINSI YA KUMTEKA MUMEO

ILI KUMTEKA MUMEO FANYA HAYA
1. Muite kwa jina lake la utani, jina lile analolipenda sana.
2. Muache atumie mamlaka yake kamakichwa cha nyumba.
3. Usimcheke akiwa ameumizwa najambo fulani.
4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira.Unaweza ukaenda kumuomba msamahana kumueleza kwanini ulimkosea palehasira zinapokua zimemuisha.
5. Kuwa na haraka ya kuomba msamahapale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.
6. Ongelea mazuri yake na yeye kablandugu, jamaa na marafiki hawajafanyahivyo.
7. Waheshimu wazazi wake. 8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia.
9. Msuprise kwa chakula akipendacho,hasa kipindi kile anapokuwa na msongowa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.
10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumiechakula mume wako ukiwa nyumbani.
11. Mkaribishe kwa kumkumbatiaanapotoka kwenye mihangaiko yake,Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.
12. Tabasamu pale unapomtizama, vaavizuri na jipendezeshe pale mnapotokawote kwenda kwenye warsha mbalimbali.
13. Mpigie simu na umwambie kwambaunampenda na umemkumbuka
14. Muamshe asubuhi na umpe romancekiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpena hata jishughulisha na wanawakewengine siku hiyo.
15. Kamwe usithubutu kutamka kuwahakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
16. Mwambie ni kiasi gani una bahatikuwa nae kama mume wako.
17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.
18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamuwako katika maisha yako.
19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhimikononi mwa Mungu.
20. Tengenezeni utaratibu wa familianzima kumshukuru Mungu kwa pamojakila asubuhi na usiku kabla ya kulala.Mungu abariki ndoa yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *