JIFUNZE KITU KUHUSU NDOA, MALI NA KIFO CHA MENGI

Walipoachana na mkewe wa kwanza aitwaye mercy Anna mengi ambaye walioana mwaka Novemba 1971 na kufanikiwa kupata watoto watatu na ukumbuke wote wawili walihusika na uanzishwaji wa makampuni ya IPP HAIKUWA RAHISI kwa mahakama kuamua kesi yao baada ya kuachana.

Mengi alikuwa akimtuhumu huyu mama wa watoto wake (mchaga wa Machame) kuwa alitaka kumuua. 
Sasa kesi ikiwa inaendelea,mahakama iliagiza makampuni yote yanayomhusisha na mkewe yafanyiwe tathimini yaani ili hizo mali zigawanywe sawa na matakwa ya mama na sheria isemavyo.
Mengi akasema hizo mali anazozisema tumenzisha wote zingine siyo kweli! 
Mengi aliiomba mahakama akutane na akae faragha na mkewe ili wakubaliane. 
Mzee akamwomba mama Regina ampe dola laki tano sawa pengine na bilioni 1 wakati huo ili wamalizane, lakini huyo mama aligoma akataka apewe dola milioni tatu karibia bilioni 7 la sivyo kesi iendelee mbele……na mengi akasema haiwezekani siwezi kukupa hiyo hela turudi mahakamani na wakairudisha kesi wakasema tumeshindwana. 
Sasa maama akaiomba mahakamani kwamba anataka hela za matumizi na matunzo kila mwezi. 
Mahakama ikaamuru awe anampa dola 40,000 kila mwezi na ndicho kiwango alichokuwa anampa kila mwezi ni kama milioni 90 hivi kwa mwezi….na hii ilichangia sana kumyumbisha kiuchumi na makampuni yake mengi.
Ni zaidi ya miaka 20 anampa milioni 90 kila mwezi. Mpaka umauti ulipomfika usiku wa kuamkia tar 1 mwezi wa 11 mwaka jana. Ndipo mzee mengi alipotoka kwenye kifungo hicho cha kutoa hizo hela huku hiyo kesi ikikosa nguvu baada ya mshtaki wa mengi au mtaliki wake kuondoka duniani baada ya kusikia hiyo taarifa ya kufariki mkewe huko Afrika Kusini hospitali ya Mediclinic Morningside, mengi alionyesha kushiriki kikamilifu kuanzia mazishi ingawaje hakumzika yeye badala yake alienda kuzikwa kwao huyo mkewe. (Machame) na mengi alihudhuria mazishi hayo ingawa
Enzi za uhai wake huyo mama aliwaambia ndugu zake “nikifa, mengi asihusike kwa lolote kwenye mazishi yangu na asichukue maiti yangu”. 
Punde baada ya mama kufariki juzi tu hapo, watoto wao, Regina na Abdiel walikwenda mahakamani na wakatangaza rasmi kuifufua kesi iliyokuwepo baina ya mama yao marehemu dhidi ya baba yao na kwamba wao ndio wasimamizi halali wa milathi ya mama yao ikiwemo ambayo wangegawana na baba yao………kwa hiyo aluta continue (mapambano yanaendelea) 
Hii taarifa mzee mengi ilimuuma sana kwamba sasa anaanza kupambana na wanae tena kwa upya ambao alishawapa tayari urithi wa biashara. 
Ni miezi mitano tu baada ya kufiwa na mama watoto wake wa kwanza…… Wakati akijipanga kuanza kula bata, maana mzee naye alikuwa hajambo kula bata…… Na yeye ndio amefariki leo. Ameacha watoto wengine mapacha kwa mkewe mdogo jackline na hana kazi nyepesi huyu mwanamke maana timbwili atayokutana nayo haineneki ingawa mzee alikumbuka wanawe hao kuwaandika kwenye mirathi yake……..na hapo juzi tu mengi alipoona wanawe wakubwa wameinuka kinyume naye akamwita na kumtambulisha mtoto wa mdogo wake kusimamia makampuni yake, nadhani alijua asingevuka huu mwezi. 

Nitakalo kulisema ni hili:
1.Chunga sana, kuwa makini na unayetaka kumwoa au kuolewa naye maana ndiye atakayeamua hatima yako iweje. Mke ni yule akupaye Mungu…….na kwenye eneo la mahusiano mzee hakuwa mfano wa kupigwa ila tunachopaswa kuiga toka kwake ni utoaji, likifika swala la kutoa mzee alikuwa anatoa pamoja na kuyumba sana kiuchumi kwenye kampuni zake. 
2.Pesa haina nafasi katika kuamua uendelee kuishi au ufe. na usijaribu kuipa nafasi kubwa moyoni mwako ila wa kumpa nafasi ni Mungu pekee. Lkn kwenye ndoa wa kumpa nafasi ni mke/mume kuliko mali.


©Patrick Patrick Chalamila

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *