Je? unajua umuhimu wa kula matango kwa wingi?

     
Wengi wetu tumekuwa tukitumia matango bila kujua yanaumuhimu gani katika miili yetu. leo nitakueleza umuhimu wa matango ambayo tumekuwa tukila kwa mara kwa mara. Kwanza kabla yakujua yote hayo tujue Tango lenye lina virutubisho gani.

Tango ni chanzo bora ya vitamini K na molybdenum. Pia ni chanzo kizuri mno cha asidi pantotheni. Pia ni chanzo kizuri cha shaba, potassium, manganese, vitamini C, fosforasi, magnesiamu, biotin na vitamini B1.

Kama ulivyoona Tango lina virutubisho vingi sana kama ilivyoelezwa hapo juu na ndipo unapoona tango lilivyo na umuhimu mwilini. kwahyo kila ulapo tango ujue umepata virutubisho vyote hvyo. baada ya kujua hayo sasa twende tukajue umuhimu wa kutumia matango.

Umuhimu wa kula matango kwa wingi

        1. Kutoa sumu mwilini (detoxification). 

Utumiaji wa matango kwa wingi husaidia kupunguza taka sumu mwilini na kufanya mwili wako kuwa na afya njema. kula angalau tango moja kwa siku ili kupunguza chemical sumu mwilini bila kusahau kunywa pia maji ya kutosha.
     

        2.Kuzuia na kupambana na kansa. 

Tango linajulikana kuwa na lariciresinol, pinoresinol na secoisolariciresinol ambazo zimekuwa zikifanyiwa utafiti kuwa zinauwezo wa kuzuia na kupambana na kansa (cancer) ambazo ni kama kansa ya matiti (breast cancer), kansa ya ovari (ovarian cancer), kansa ya kizazi (uterine cancer) na kansa ya prostati (prostate cancer).

        3.kutatua tatizo la kunuka mdomo(bad breath).

Tango lina kemikali ijulikanayo kama phytochemcials ambayo inauweza wa kuuwa bacteria waletayo arufu mbaya mdomoni. chukua kipande cha tango na kiweke kwenye kuta za juu za mdomo kwa sekunde 30.

 

       4. kupunguza uzito na kusaidia kumeng’enya chakula.

Kwa wale ambao wanataka kupunguza uzuti kunanjia nyingi za kukabiliana na swala hilo na tango ni diet nzuri kwa mtu ambaye anatatizo la uzito kwakuwa tango lina kalori kiasi kidogo mno na pia lina maji ya kutosha ambayo ni muhimu katika kuongeza maji mwilini. Bofya hapa kuziju njia rahisi za kupunguza uzito wa mwili na kuwa na afya bora.

       5. Kusaidia watu wenye kisukari (Diabetes).  

Tango lina chemical ambazo zinaitajika kwenye cell za kongosho (pancrease) ilikutengeneza insulini ambayo inasaidia kupunguza na kubalance sukari mwilini

     6. Inasaidia joints na gout.

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha silica ambayo husaidia kuimarisha joint za magoti. Matango yamekuwa ya muhimu sana kwa wale wenye matatizo ya magoti, gout na arthritis kwa kuwa yana kiwango kikubwa cha vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na Potassium. Na hufanya kazi vizuri yanpotumia kwa pamoja na karoti.

 KAMA UNA JUA AU UNATAARIFA ZAIDI KUHUSU UMUHIMU WA MATANGO USISITE KUSHARE NASI KWA KUCOMMENT HAPO CHINI NA PIA KAMA UNASWALI PIA USISITE KUULIZA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *