HIVI NDIVYO UTOFAUTI ULIPO KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME KATIKA HISIA ZA KIMAPENZI

 • Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya kimapenzi. Hata hivyo kutokana na nguvu ya mahusiano,,, watu wengi hufikiri wanaume ndiyo ambao wanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na nguvu hiyo… 
 •  Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba,, Mwanaume kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana na wanaume wengi hupenda sana jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndiyo maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia  zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.  
 • (Mfano.. Hivi hujawahi kuona wanaume wakiwa wamekaa wakipiga story,, gafla apite mwanamke mzuri mrembo na mwenye kuvutia hisia mbele ya macho yao. Gafla story zile lazima zisimamishwe)  Bila shaka umewahi kuona mfano huo. Au utawasikia wakinong’onezana “,Aaah…!! Tazama kifaa hicho kinapita , wengine utawasikia,,, muone chura. Hii inamaana ya kwamba macho ya mwanaume ndiyo chanzo kikubwa cha kuingia kwenye mahusiano kabla ya kujua tabia ya huyo mtu. 
 • Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi huingia katika matamanio kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema, matamanio ya hisia za mwanaume  yapo katika kuona katika kuona zaidi kuliko kitu chochote. 
 • Lakini ukienda sehemu ya Pili. ##Mwanamke yupo tofauti sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso kutoka kwa Mwanaume, hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na Mwanaume. 
 • Mwanamke huamini sana katika kuambiwa maneno na mwanaume,  Kwa mfano: (Mwanamke akiambiwa anapendwa sana zaidi ya kitu chochote katika dunia hii ) mwanamke huamini kwa asilimia moja… Hivyo mwanaume ana nafasi kubwa ya kuziteka hisia za mwanamke. 
 •  Lakini pia hiyo kama haitoshi. Mwanamke hupata hisia kubwa pale anapoguswa na mwanaume, hivyo maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza,,, ataki umguse katika mwili wake ,,,hii inamaana kwamba mguso wa Mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke. 
 • Tambua hilo kwa sasa. hivyo ndivyo utofauti mkubwa kati ya mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi.. 
 •     Na kitu kikubwa ambacho huongeza hamasa, na hudumu katika mahusiano ya kimapenzi ni (MAWASILIANO)   Mawasiliano ndiyo chachu kubwa sana katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu . Hakikisha mnakuwa na mawasiliano bora kati yako na muenzi wako. ….
 •  *ASANTENI,* 

One Comment

 1. I loved as much as you’ll receive carried out right here.
  The sketch is tasteful, your authored subject matter stylish.
  nonetheless, you command get bought an nervousness over that you wish be delivering
  the following. unwell unquestionably come further formerly again as exactly the same nearly a lot often inside case you shield this increase.
  http://Www Vintagehouserestaurant com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *