HASARA ZA KUJIPENDEKEZA KWA MTU

Soma hii ujifunze kitu… ✍🏽1.. Hauwezi kumkemea huyo unayejipendekeza kwake hata kama anakosea… 2.. Unakuwa mtumwa kwa huyo unayejipendekeza kwake.   3.. Unafanya akili yako ishindwe kuzalisha matunda maana unakuwa tegemezi kwa huyo unayejipendekeza kwake.. 4.. Utajikuta unakosana na watu hasa wakimkosoa huyo unayejipendekeza kwake. Maana hutokubali akosolewe mbele yako. 5.. Inakufanya kuwa mnafiki, maana hata wewe kwenye ndani ya moyo wako kuna vitu havipo sawa anakosea. Lakini unamezea tu ili kulinda kufukuzwa.. 6.. Inakuharibu kisaikolojia, hasa pale ambapo hautapata kile ulichokitegemea kwa huyo unayejipendekeza kwake… 7.. Inakufanya uyanyonge maono uliyonayo kwa mikono yako mwenyewe. Maana muda mwingi unatafuta jinsi yakumpendeza huyo unayejipendekeza kwake,  badala ya kuwekeza muda wako kwenye maono binafsi.. 8.. Kuna kufanya huyo unayejipendekeza kwake awe “Mungu mtu” Hivyo unajikuta unamsujudia kwa kila jambo.. 9.. Hauwezi kufanya maamuzi binafsi, ni mpaka huyo unayejipendekeza kwake ndio aje akuamulie. Akikataa ndio basi. 10.. Utagombana na watu mara kwa mara, maana kila atakayejionyesha kuwa karibu na huyo unayejipendekeza kwake. Unaweza ukampiga hata mawe maana utafikiri abaichukua nafasi yako.. 11..Inakufanya uthamani wako ushuke kabisa na kudharaulika, maana unaishi kwa kumtegemea mwanadamu mwenzako bila ya yeye haukai mjini. 12.. Hauwi mwanaume halisi au mwanamke halisi. Maana walio halisi wanamisimamo binafsi na waka hawayumbi, kama ulivyo wewe kwa huyo unayejipendekeza kwake maana umekuwa kama bendera kufuata upepo.. 
 Ushauri… ✍🏽

  1. Acha kujipendekeza kwa watu sana, watakuona wewe umjinga na huna cha kuwaambia kutoka katika kauli yako. Bali wao ndio wenye kauli za kukwambia, na kukutumisha kwa vitu vyengine visivyofaa hapo baadae. 
  2. Tambua kwamba unapojipendekeza kwa mtu, jua kwamba unajishusha hadhi yako wewe mwenyewe. Kuwa mjasiri wa kuongea vitu ambavyo huvipendi kwake, kuwa mkimya kwa mtu unayejipendekeza kwake kwa sababu amekosea kitu. My Friend utakuja kuniambia hapo baaade, hata kama amekuajiri kikazi haimaanishi ndio uzubae na kujipendekeza kwake sana tambua kwamba utakuwa mtumwa siku zote… Zingatia hili… 

*Kama umeipenda hii na imekufunza kitu, basi share kwa magroup mengine na marafiki zako wapate faida…*Ukihitaji ushauri wowote unaweza ukaacha comment happy chini. *NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO KWAKO NA KWETU SOTE.. 🤲🏽*

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *