FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI/MGOLO

🍀 *BAWASIRI/MGOLO* 🍀
⚡Bawasiri ni ugonjwa unaotokea katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama piles.Na kitaalam hujulikana kama hemorrhoids
🍃AINA ZA BAWASIRI🍃
 • 👉1⃣ BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina hii ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
 • 👉2⃣BAWASIRI YA NDANI 
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu. 
Aina hii imeainishwa katika mainisho ya madaraja manne yafuatayo:
 1. 👉Daraja la 1 – Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida   
 2. 👉Daraja la 2 – Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya haja.
 3. 👉Daraja la 3 – Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya haja. N.k
   BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
 • 👉Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
 • 👉Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
 • 👉Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
 • 👉Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
 • 👉Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
 • 👉Kuharisha sana kwa muda mrefu
 • 👉Kutumia vyoo vya kukaa
 • 👉Kunyanyua vyuma vizito
 • 👉Mfadhaiko/stress
 • 👉Uzito na unene kupita kiasi.

🌱DALILI ZA BAWASIRI🌱

 • 👉Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
 • 👉Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
 • 👉Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
 • 👉Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
 • 👉Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *