BARUA YA MAMA KWENDA KWA MWANAYE – SIKU TATU BAADA YA MAZISHI

Mpendwa mwanangu,

Nataka ujue kwa nini nilikufa nikiwa masikini wakati nina mtoto kama wewe.
Mwanangu, nilitaka kukupa baraka zangu kabla sijafa, lakini sasa nimeondoka na baraka zangu.
Chakula changu cha asubuhi, cha mchana na cha usiku kilikuwa miongoni mwa changamoto zangu nilipokuwa hai, lakini wewe umetumia pesa kupika kila aina ya vyakula, nyama na  kununua aina mbalimbali za vinywaji siku ya mazishi yangu.
Mwanangu, ulichagua kuupaka mwili wangu uliokufa kwa kutumia mafuta mazuri na manukato yenye kunukia wakati nilipokuwa hai nilitumia mawese kujipaka kwa kukosa mafuta.
Umeivika maiti yangu kwa nguo ghali wakati ulishindwa kuninunulia hata khanga.
Maiti yangu ilipokuwa mochwari ulikuja kunitazama mara kwa mara, kwa nini umeijali maiti yangu wakati ulishindwa kunijali nilipokuwa hai?
Kitu kinachoniuma zaidi ni jeneza la bei kubwa ambalo umeuweka mwili wangu ilhali nilipokuwa hai The most painful niliishi katika nyumba mbovu ambayo haikumaliziwa kujengwa.
Ulipokuwa mdogo nilikaa na njaa ili wewe ule na kushiba, nilivaa nguo kuukuu ili upate nguo za kutosha. Nilidhani utanitunza nikizeeka.
Wakati wa mazishi yangu ulimalizia nyumba, ukaipaka rangi na kuusafisha uwanja ndani ya wiki moja ili tu upate kuadhimisha mauti yangu.
Sasa umeniandikia tanzia ukisema “Mama, nakupenda sana, pumzika kwa amani” – ilhali nimekufa nikiwa na maumivu moyoni.
 
Mwisho kabisa, mwanangu, nimekuandikia kukukumbusha kuwa hakuna mtu anayempenda mtoto kama mama yake.
Mungu akusamehe.
—————————————
Tafadhali shea ujumbe huu uwafikie watu wengine ili waweze kuwajali watu wakiwa hai badala ya kuwajali wakiwa wamekufa.
Wajali sana wazazi wako wakati wakiwa hai. MAMA MKWE
Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya.
MUME: Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama hajisikii vizuri. Tunaweza kwenda kumnunulia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kumtembelea? Tafadhali andika orodha ya mahitaji kisha tuondoke.
MKE: Orodha ya vitu hivyo sio muhimu, tutanunua tu kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia.
MUME: Vitatosha kweli?
MKE: Ndiyo mpenzi, hakuna haja ya kupoteza pesa, vitatosha.
Walielekea mjini na kununua kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia. Wakati wakinunua mume alimuuliza mkewe tena kama vitu hivyo vingetosha.
Mke alisisitiza zaidi kuwa hawatakiwi kutumia pesa nyingi kwenye ziara ya kushtukiza.
Walianza safari kuelekea kijijini, na walipofika kwenye eneo la njia panda yenye barabara zinazoelekea vijiji mbalimbali, mume alikata kona kuelekea kwao na mke.
MKE: (Kwa mshituko) tunaelekea wapi mpenzi?  Nilidhani tunaenda kumtembelea mama yako.
MUME: Ndiyo, ndiko tunakuelekea. Ni mama yako (mama yetu) ndiye anayeumwa.
MKE: (kwa mshituko na kilio), lakini mahitaji haya hayatoshi. Turudi tuongeze vitu vingine.
MUME: Hapana! Nilikuuliza tena na tena kama mahitaji hayo yanatosha, ukaniambia “NDIYO”. Hakuna kurudi…..
FUNZO:
Wafanyie wenzako kile unachotaka ufanyiwe!!
Tunawatakia ndoa maridhawa isiyokuwa ya mwendo kasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *